Polisi Iraq wadai kumkamata Khaldoon

0
587

Polisi nchini Iraq wamesema kuwa, wamemkamata Makamu Mkuu wa kikundi cha IS kilichokuwa kikiongozwa na Abou Bakri Al Baghdad, ambaye majeshi ya Marekani yalidai kumshambulia nchini Syria.

Mtu huyo Abu Khaldoon amekamatwa katika mji wa Hawijah, baada ya polisi nchini Iraq kufanya upekuzi wa kushitukiza katika mji huo.

Marekani imesema kuwa Al Baghdad akiwa na watoto Wawili aliamua kujilipua na kujiua akiwa ndani ya handaki, baada ya kubaini kuwa majeshi ya Marekani yalikuwa yakimkimbiza yakiwa na mbwa, na handaki hilo lilikuwa halina mahali pa kutokea.

Kikundi cha IS kimekuwa kikihatarisha usalama katika maeneo mbalimbali duniani kwa kuhusika na mashambulio ya kigaidi, kikiwa na lengo la kuanzisha utawala wa Kiislamu katika maeneo kinayotwaa.