Amin kuwania nafasi ya juu CECAFA

0
803

Rais wa Chama Cha Soka cha Sudan Kusini (SSFA) Francis Paul Amin,
ametangaza rasmi kuwania nafasi ya Umakamu wa Urais wa Baraza la Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Amin amekuwa akipigiwa upatu na baadhi ya Wadau wa Soka wa ukanda wa CECAFA kuwania uongozi kwenye Baraza hilo kutokana na mipango yake mizuri ya kuboresha soka nchini mwake.

Soka la Sudan Kusini kwa siku za hivi karibuni limepiga hatua kubwa kutokana na mipango na mikakati mizuri anayoifanya Kiongozi huyo, na hicho ndicho kitu kikubwa kilichowashawishi baadhi ya Viongozi wa Soka wa ukanda wa CECAFA kumtaka aingie ndani ya Baraza hilo.

Uchaguzi mkuu wa CECAFA utafanyika Tarehe 18 wezi huu katika jiji la
Kampala nchini Uganda