Halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi inakusudia kukagua magari yanayoingia wilayani humo ili kubaini na kudhibiti uingizaji wa Korosho zenye ubora hafifu katika soko la Kilwa.
https://www.youtube.com/watch?v=zNEBAQj6t-A&feature=youtu.be
Akizungumza mara baada ya kikao cha Baraza la Madiwani katika Mji Mdogo wa Masoko, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Abuu Mjaka amesema kuwa, kumekuwa na uingizwaji wa Korosho zisizo na ubora katika halmashauri hiyo hali inayosababisha kushuka kwa Soko la Korosho zinazotoka wilayani Kilwa.