Bondia Mwakinyo ampiga Tinampay kwa pointi

0
916

Bondia Mtanzania,- Hassan Mwakinyo amepata ushindi dhidi ya bondia Arnel Tinampay kutoka nchini Ufilipino, kwenye pambano la raundi Kumi lililofanyika katika dimba la Uhuru jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwakinyo ambaye ni Bondia kutoka mkoani Tanga amesema kuwa, anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kushinda mpambano huo licha ya changamoto kadhaa alizokutana nazo.

Ameongeza kuwa, kwa sasa Tanzania inachohitaji ni kuja kwa Wanamasumbwi Manny Pacquiao pamoja na Amir Khan.

Katika mpambano huo ulioshuhudiwa na mashabiki kutoka maeneo mbalimbali, Jaji wa kwanza ametoa pointi 97-93, Jaji wa Pili 98-92 na Jaji wa Tatu ametoa pointi 96-96.

Pambano hilo lilitanguliwa na mapambano mengine likiwemo lile lililompa ushindi wa pointi Mfaume Mfaume dhidi ya Keisi Ally.