Waziri Mhagama aagiza kukamilika kwa kiwanda cha ngozi

0
390

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama ameuagiza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Jeshi la Magereza, kuhakikisha ujenzi wa kiwanda cha ngozi cha Karanga kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro unakamilika ifikapo Januari 20 mwaka 2020.

Waziri Mhagama ameyasema hayo wakati alipotembelea kiwanda hicho na kuongeza kuwa, Serikali inatamani kuona kiwanda kicho kikifanya kazi kwa kuwa malighafi ya ngozi ambayo itatengeneza bidhaa za ngozi ipo kwa wingi.

Ameongeza kuwa, mbali na hilo, kiwanda hicho kitasaidia kuwapa ajira vijana kuanzia Elfu Mbili hadi Elfu Nne pamoja na kupata fedha za kigeni kwa kuuza viatu nje ya nchi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , – Andrew Massawe ameahidi kufuatilia na kuhakikisha ujenzi wa kiwanda hicho unakamilika kamawalivyoagizwa.