Suala la udhalilishaji katika vyumba vya habari lavaliwa njuga

0
222

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amewaagiza Maafisa wa wizara yake kutengeneza namba maalum ya kupokea malalamiko ya ukatili wa kijinsia unaofanyika katika vyumba vya habari. 

Dkt Mwakyembe ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam, wakati wa warsha ya kujadili nafasi ya Mwanamke katika vyumba vya habari ambapo amewasisitiza Wanawake kutoyafumbia macho matukio ya udhalilishaji wa kijinsia yanayofanywa na baadhi ya Wahariri wa habari.

Warsha hiyo imefanyika pamoja na uzinduzi wa kitabu cha Jinsia na Habari, kitabu kilichoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake UN WOMEN.