Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema TANZANIA inahitaji watendaji wa sekta ya uvuvi kuanzia ngazi ya vitongoji kwani kuna vijiji vina mito, maziwa na baadhi vimepakana na bahari na hivyo kutoa fursa za uvuvi.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jijini DSM wakati akizungumza na wahadhiri na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DSM Kampasi ya KUNDUCHI.
Amesema angependa kuona watafiti na watalaam wanapewa fursa ya kuongoza na kusimamia maeneo yanayohusiana na utafiti walioufanya ili kupata matokeo sahihi ya utafiti wao.