Nchi za EAC zatakiwa kushirikiana kuimarisha Jumuiya hiyo

0
223

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa
Palamagamba Kabudi amezishauri nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ( EAC) kushirikiana kuiimarisha Jumuiya hiyo kwa maslahi ya
Wananchi wa Afrika Mashariki.

Profesa Kabudi ametoa ushauri huo jijini Arusha wakati wa mkutano mkuu wa Biashara na Uwekezaji wa Afrika Mashariki, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya EAC.

Pia amewataka Wafanyabiashara katika nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza katika biashara zinazoleta matokeo chanya kwa jamii husika.

Akimwakilisha Katibu Mkuu wa EAC Balozi Liberat Mfumukeko, – Naibu
Katibu Mkuu Uzalishaji kutoka Jumuiya hiyo Christopher Bazivamo amesema kuwa, licha ya mafanikio yaliyopatikana katika miaka 20 ya Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki, bado kuna changamoto mbalimbali zikiwemo zile za uchache wa Viwanda na mitaji ya kuanzisha biashara kwa Wananchi.