Lindi yazindua Mwongozo wa Uwekezaji

0
2715

Mkuu wa mkoa wa Lindi, -Godfrey Zambi amesema kuwa, mkoa huo umejipanga kuhakikisha Wawekezaji wanaotaka kuwekeza mkoani humo wanafanya kazi katika mazingira rafiki.

Zambi ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji kwa mkoa wa Lindi, uzinduzi uliohudhuriwa na Wadau mbalimbali katika masuala ya Uwekezaji.

Ameongeza kuwa, mkoa wa Lindi una maeneo mengi ya Uwekezaji hasa katika Viwanda, Kilimo na Utalii, na hivyo kuwakaribisha Wawekezaji kwenye maeneo hayo kwenda kuwekeza.

Mkuu huyo wa mkoa wa Lindi ameahidi kuwapa ushirikiano Wawekezaji wote waliionyesha nia ya kutaka kuwekeza katika sekta mbalimbali mkoani humo.