Askari 13 wa Ufaransa wamekufa katika ajali nchini Mali

0
690

Askari Kumi na Watatu wa Jeshi la Ufaransa wamekufa baada ya helkopta waliyokua wakitumia katika operesheni za kijeshi dhidi ya Wanamgambo nchini Mali kuanguka.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Ufaransa imeeleza kuwa, Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo amesikitishwa na tukio hilo na kutaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina ili kufahamu kama kulikua na njama zozote zilizosababisha kuanguka kwa helkopta hiyo.

Tangu mwaka 2012, Mali imekua ikikumbwa na mapiganio ya mara kwa mara hasa baada ya Wanamgambo hao kuchukua udhibiti katika eneo la Kaskazini.

Askari wa Ufaransa wapo nchini Mali kuvisaidia vikosi vya nchi hiyo katika operesheni za kukabiliana na Wanamagabo hao hasa katika eneo hilo la Kaskazini.