“Isidingo: The need” yapigwa kibuti

0
2012

Kumekuwa na fununu za hapa na pale kuwa tamthilia ya muda mrefu “Isidingo: The need” imepigwa kibuti kuoneshwa na SABC 3

Isidingo ni tamthilia kutoka Afrika Kusini, inayorushwa na kituo cha televisheni SABC 3 ambayo inatakriban watazamaji 980,000

Licha ya kuongeza kiwango cha mauzo ya SABC3 mara kwa mara imekuwa na mvuto kwa watazamaji lakini kupitia gazeti la Sunday World limetoa sababu zakusitishwa Tamthilia hiyo ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa wasanii mahiri na kukosa mvuto wa kutokuwa Tamthilia inayoongoza tena SABC 3 kwa sasa.

Sababu nyingine ya kusimamishwa ni kutovutia matangazo kwajili ya biashara

Julai mwaka huu Isidingo imesherekea mwaka wa 21 kurushwa katika TV

Walipowasiliana na afisa mawasiliano wa uandaaji wa “Isidingo” alikataa kutoa maoni, lakini akasema watatoa kwa wakati muafaka.

“Kampuni haina maoni. Tutatoa taarifa kwa muda wake,” amebainisha Catherine Sidyiyo

Wapenzi na mashabiki wa “Isidingo” kupitia kurasa za twitter wametoa maoni yao na kupinga kusitishwa kwa Tamthilia hiyo.