BODI ya FILAMU yawageukia Wenye Mabasi

0
230

BODI ya Filamu Nchini imevitaka Vyombo vya usafiri hususani Mabasi ya Abiria yaendayo mikoani kutoonyesha kanda za video ikiwa ni pamoja filamu au miziki mpaka ijiridhishe kuwa kanda hiyo imepitia katika Bodi hiyo na kupatiwa Kibali.

Wito huo umetolewa Jijini Dar as salaam na Kaimu Katibu Mtendaji wa bodi hiyo Dokta Kiagho Kilonzo akisema miongoni mwa kanda ambazo haziruhusiwi kuonyesha ni pamoja na kanda zinazoonyesha hali ya kibaguzi, Kanda inayochafua taswira ya mtu, kanda inayoonyesha tupu za mtu pamoja na kanda zinazochochea uvunjifu wa amani.