Sitaki askari wabebe mzigo wa kulipa deni : Rais Magufuli

0
226

Serikali imeahidi kulipa deni la zaidi ya Shilingi Trilioni Moja kama pango la nyumba  linalodaiwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), deni   ambalo limekua likikatwa kwa askari wanaoishi  kwenye nyumba 6,600 zilizojengwa kwa ajili ya Jeshi hilo.

Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa katika eneo la Kikombo, -Chamwino mkoani Dodoma, Rais John Magufuli amesema kuwa, tayari amemuelekeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango pamoja na Katibu Mkuu Hazina Doto James namna ya kufanya kuhusu deni hilo.