Ajali ya ndege yaua 24 DRC

0
701

Watu 24 wamethibitika kufa, baada ya ndege ndogo ya abiria kuanguka katika makazi ya watu kwenye mji wa Goma uliopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Habari kutoka DRC zinaeleza kuwa, ndugu Wanne wa familia Moja ni miongoni mwa watu waliofariki Dunia baada ya nyumba yao kuangukiwa na ndege hiyo.

Ndege hiyo ndogo imeanguka jirani kabisa na uwanja wa ndege uliopo kwenye mji huo baada ya kushindwa kupaa.

Wakati ajali hiyo inatokea, ndege hiyo ilikua na abiria 17 pamoja na Wafanyakazi Watatu.

Ajali za ndege katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo zimekua zikitokea mara kwa mara kutokana na kutokuwepo kwa ufuatiliaji wa kutosha katika safari hizo pamoja na kutokuwepo kwa matengenezo kwa baadhi ya ndege.