Takribani watu Arobaini wanadhaniwa kufa nchini Kenya, baada ya nyumba zao kusombwa na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo.
Habari zaidi kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa, watu wengine Thelathini hawajulikani walipo kufuatia maporomoko hayo ya udongo.
Vikosi vya Uokoaji na Zimamoto nchini Kenya vimesema kuwa, hali ni mbaya zaidi katika eneo la Pokot na kwamba kinachoendelea hivi sasa ni kutafuta Miili ya watu wanaodhaniwa kufa katika tukio hilo.
