IGP aagizwa kuwasimamisha kazi Kamanda wa Polisi na Mkuu wa Upelelezi Shinyanga

0
296

Rais John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro, kumsimamisha kazi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, -Richard Abwao na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Shinyanga,- John Rwamlema kufuatia tuhuma za utovu wa nidhamu na kuhusika katika uhujumu uchumi zinazowakabili.

Halikadhalika Rais Magufuli amemuagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt Edwin Mhede kumsimamisha kazi Meneja wa TRA mkoa wa Shinyanga, – Jumbe Samson kutokana na tuhuma za kuhusika katika uhujumu uchumi.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu imeeleza kuwa, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma zinazowakabili viongozi hao.