Kauli ya Waziri Jafo kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa

0
220

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),- Selemani Jafo amewataka Wananchi waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuzingatia Kanuni na Sheria za uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kujiepusha na uvaaji wa sare za vyama vya siasa katika zoezi la kupiga kura.

Waziri Jafo amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo hapo kesho.

Amesema kuwa, mambo yote muhimu kuhusu uchaguzi huo yamekua yakisisitizwa katika muda wote mchakato wa uchaguzi ulipokua ukiendelea, hivyo ni vema mambo hayo yakazingatiwa ili kuhakikisha Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa unafanyika katika mazingira ya Amani na Utulivu.

Mikoa ambayo haitafanya uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ni Njombe
Tanga, Katavi na Ruvuma, na ni baada ya Wagombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupita bila kupingwa.