Rais mpya wa Sri Lanka, -Gotabaya Rajapaksa amesema kuwa, ataitisha uchaguzi wa Bunge mwezi Machi mwaka 2010 kufuatia ushindi wake wa kishindo.
Rais Rajapaksa anatarajiwa kuitisha uchaguzi huo miezi Sita kabla ya muhula wa miaka Mitano ya Bunge la sasa kukamilika.
Hata hivyo Gotabaya amesema kuwa, atashauriana na Raia wa nchi hiyo ili kubaini wakati muafaka wa kuandaa uchaguzi huo mapema iwezekanavyo kwa mujibu wa Katiba.
Rais Gotabaya ameyasema hayo mara baada ya kuliapisha Baraza jipya la Mawaziri la Sri Lanka linaloongozwa na Kaka yake Mahinda Rajapaksa, ambaye ni Rais wa zamani wa nchi hiyo lakini kwa sasa atahudumu kama Waziri Mkuu pamoja na waziri wa fedha.
