Rais mpya wa Sri Lanka,- Gotabaya Rajapaska amemuapisha Kaka yake Mahinda Rajapaska kuwa Waziri Mkuu wa Mpito wa nchi hiyo.
Mahinda ameapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Colombo.
Gotabaya Rajapaska alichaguliwa kuwa Rais mpya wa Sri Lanka katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita na kusema kuwa katika uongozi wake atahakikisha haki za Raia wote wa nchi hiyo zinalindwa.
Mahinda Rajapaska aliwahi kuutumikia wadhifa wa Urais wa Sri Lanka kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2015, wakati huo Gotabaya akiwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo.
