Rais John Magufuli muda mfupi ujao atatunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Rais Magufuli anatunukiwa Shahada hiyo wakati wa mahafali ya Kumi ya UDOM, ambapo yeye ni mgeni rasmi.
Mahafali hayo yanahudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai pamoja na Viongozi Wastaafu.
