Mkurugenzi Mkuu NIDA aagizwa kwenda Morogoro haraka

0
237

Rais John Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), -Dkt Arnold Kihaule kwenda mkoani Morogoro hii leo, ili kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi wakati wa kujiandikisha kupata Vitambulisho vya Taifa.

https://www.youtube.com/watch?v=oPoJ1g7wx6M

Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Wakazi wa mkoa wa Morogoro, baada ya baadhi yao kulalamika kuwa, wamekua wakikutana na changamoto kadhaa wakati wa ufuatiliaji wa Vitambulisho hivyo vya Taifa.

Ameagiza zoezi za usajili Wananchi kwa ajili ya kupata Vitambulisho hivyo lifanyike katika wilaya zote za mkoa wa Motogoro na kwa haraka , ili Wananchi hao waweze kutumia Vitambulisho hivyo katika kusajili laini zao za simu za mkononi.

Rais Magufuli amesema kuwa, haiwezekani watu kutumia muda mrefu na kusafiri mbali mrefu kutoka eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya kusajiliwa kupata Vitambulisho vya Taifa, wakati kuna uwezekano wa kupata huduma hiyo katika maeneo yao.

Wakitoa malalamiko yao kwa Rais Magufuli, baadhi ya Wakazi wa mkoa wa Morogoro wamesema kuwa, wamekua wakitumia hadi siku Tatu kufuatilia Vitambulisho hivyo vya Taifa katika Ofisi za NIDA za mkoa.

Rais Magufuli amezungumza na Wakazi hao wa mkoa wa Morogoro, akiwa njia kuelekea jijini Dodoma.