Taifa Stars wakubali kichapo Ugenini

0
1189

Timu ya Taifa ya Tanzania imekubali kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Timu ya Taifa ya Libya katika mechi za makundi kufuzu AFCON 2021

Hadi mapumziko Taifa stars ilikuwa inaongoza kwa bao moja bila bao likifungwa na Nahodha Mbwana Samatta kwa mkwaju wa penati

Libya wakatumia vizuri udhaifu wa safu ya ulinzi ya Taifa Stars na kurudisha bao la kwanza kupitia kwa Masoud akipiga mkwaju wa penalt uliomshinda golikipa Juma Kaseja

Baada ya mashambulizi mengi langoni kwa Taifa Stars Libya wakaongeza bao la pili na kuifanya Tanzania kupoteza mchezo huo wakiwa ugenini