Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya yaendelea

0
210

Taasisi mbalimbali na Jamii wameshauriwa kushirikiana katika kutoa elimu kuhusu athari za dawa za kulevya, na hivyo kuokoa nguvu kazi kubwa ya Taifa inayoweza kuathirika kwa matumizi ya dawa hizo.


Ushauri huo umetolewa jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini James Kaji, wakati wa uzinduzi wa banda maalum la kutolea elimu kuhusu athari za dawa za kulevya kwenye eneo la soko la Samaki la Feri.