Wanaopatiwa mikopo watakiwa kuirejesha

0
223

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es salaam, -Sarah Msafiri, amewataka wanufaika wa mikopo inayotolewa na Halmashauri kuwa waaminifu katika urejeshaji fedha, ili waweze kuwa na sifa ya kukopeshwa kwa mara nyingine.


Msafiri amesema hayo wakati akikabidhi hundi za mikopo yenye thamani ya Shilingi Milioni 300 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Wenye ulemavu katika halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.


Wajasiriamali 880 watanufaika na mikopo hiyo, ambayo ni sehemu ya asilimia Kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo ya Kigamboni, na hurejeshwa bila ya riba tofauti na ile ya taasisi nyingine za kifedha.