Uturuki imesema kuwa itaanzisha upya operesheni za kijeshi Kaskazini Mashariki mwa Syria, iwapo Wapiganaji wa Kikurdi hawataondoka katika eneo la mpaka wa nchi hizo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, – Mevlut Cavusoglu baada ya kubaini kuwa Marekani na Russia hazijatekeleza makubaliano yaliyositisha operesheni hizo za kijeshi za Uturuki dhidi ya Wapiganaji wa Kikurdi.
Cavusoglu amezitaka Marekani na Russia kutimiza wajibu wao kwenye makubaliano yaliyofikiwa, vinginevyo operesheni hizo za kijeshi zitaanza muda wowote kuanzia sasa.
Chini ya makubaliano hayo baina ya Uturuki, Marekani na Russia, Wapiganaji hao wa Kikurdi ambao ni washirika wa Marekani, walitakiwa kuondoka kutoka eneo la Kaskazini Mashariki mwa Syria, eneo ambalo ni mpaka wa nchi hiyo na Uturuki.