SIDO yapata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka Minne

0
174

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), limepata mafanikio makubwa katika miaka Minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano, ikiwa ni pamoja na kuweka mpango wa kuwapatia ujuzi vijana katika masuala ya ufundi.

Akizungunza katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Profesa Sylvester Mpenduji amesema kuwa, katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuwa na uchumi wa Kati, SIDO imejenga majengo 12 kwa ajili ya uwekezaji katika Viwanda vya aina mbalimbali.