Swahili Fashion Week kufanyika Disemba

0
1685

Maonesho ya mavazi ya Swahili Fashion Week yanatarajiwa kufanyika Disemba Sita, Saba na Nane mwaka huu katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Maonesho hayo yanafanyika kwa mara ya 12 ambapo pia zitatolewa Tuzo katika vipengele 26, kwa ajili ya kutambua mchango wa Wadau mbalimbali kwenye tasnia ya ubunifu.

Pamoja na mambo mengine, wakati wa maonesho hayo ya mavazi ya Swahili Fashion Week kutakua na mauzo ya wazi ya mavazi mbalimbali.

Wabunifu 34 wa mavazi kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na katika Mataifa mengine Duniani, wataonyesha vipaji vyao wakati wa maonesho hayo.

Onesho la mavazi la Swahili Fashion Week, limekua likifanyika kila mwaka ambapo Wabunifu wa mitindo na Warembo kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili na nchi nyingine Duniani wanatumia fursa hiyo kuonyesha vipaji vyao pamoja na kuuza ubunifu wao.

Muasisi wa Swahili Fashion Week, – Mustafa Hassanali ametoa wito kwa Watanzania kupenda kuvaa mavazi yaliyobuniwa na Wabunifu wa Tanzania ili kukuza vipaji pamoja na vipato vyao.