Kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu zinaanza hii leo katika maeneo mbalimbali nchini.
Kampeni hizo zinafanyika kwa muda wa siku Saba, ambapo vyama mbalimbali vya siasa vinavyoshiriki kwenye uchaguzi huo vitapata nafasi ya kuwanadi Wagombea wao pamoja na Sera zao.
Tayari mchakato wa kuelekea katika uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa umepita kwenye hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na uandikishaji Wapiga kura, uchukuaji wa fomu na urejeshaji wa fomu hizo kwa Wagombea na Uteuzi wa Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.
Katika maelekezo yake kwa vyama mbalimbali vinavyoshiriki uchaguzi huo, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imevitaka vyama hivyo kuhakikisha vinafuata taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha kampeni hizo zinafanyika katika hali ya amani na utulivu.
