Dkt Jingu amfariji Mtoto Anna

0
267

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt John Jingu, leo amefika Goba mkoani Dar es salaam ambako ni nyumbani kwa familia ya Mtoto Anna Zambi mwenye umri wa miaka 16, ambaye Wazazi wake wote Wawili pamoja na wadogo zake Watatu wamefariki Dunia, ili kumpa pole na kumfariji mtoto huyo kutokana na msiba huo mkubwa.

Wazazi wa Anna, -Lingston Zambi na Winifrida Lyimo pamoja na ndugu zake Watatu Lulu, Andrew na Grace walifariki Dunia Oktoba 26 mwaka huu wakiwa njiani kutoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro, kwenye Mahafali ya Kidato cha Nne ya Anna, ambapo gari walilokua wakisafiria lilisombwa na mafuriko huko Handeni mkoani Tanga.