Waziri wa Kilimo,- Japhet Hasunga ameitaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kufanya ukaguzi wa kina katika Mfuko wa Kuendeleza Zao la Korosho (WAKFU) ili kujiridhisha na matumizi ya Shilingi Bilioni 53.2 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa viwanda Vitatu vya kubangua Korosho pamoja na maghala.
Akizungumza na
Waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri Hasunga amesema kuwa, Serikali imefikia uamuzi huo kwa kuwa inataka kufahamu namna fedha hizo zilivyotumika.
Waziri huyo wa Kilimo amesisitiza kuwa, Serikali itachukua hatua kali kwa wahusika wote endapo ukaguzi huo wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali utaonyesha kuwepo kwa ubadhirifu katika matumizi ya fedha hizo.
