Morales ataka kusuluhishwa mgogoro wa kisiasa Bolivia

0
754

Aliyekuwa Rais wa Bolivia, – Evo Morales ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa ama Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francis, kusuluhisha mgogoro wa kisiasa uliomlazimu kujiuzulu na kukimbilia uhamishoni nchini Mexico.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika mji Mkuu wa Mexico, – Mexico City, – Morales amesema kuwa, anaamini yeye bado ni Rais wa Bolivia kwa sababu Bunge la nchi hiyo halijaridhia barua yake ya kujiuzulu.

Wakati wa mkutano huo, Morales amesisitiza nia yake ya kurejea nchini Bolivia kutoka uhamishoni nchini Mexico.

Wakati hayo yakiendelea, Rais wa Mpito wa Bolivia, – Jeanine Anez amezuia Morales kugombea kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu ujao na kusema kuwa, Morales hawezi kufanya hivyo kwa kuwa Katiba ya Bolivia inazuia Rais kuongoza kwa zaidi ya mihula miwili mfululizo.