Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amezindua Mpango Mkakati wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ambukiza nchini, akiwataka watanzania kuepuka visababishi vya maradhi hayo jambo ambalo pia litasaidia kuokoa bajeti kubwa ya Wizara ya Afya katika kuyakabili maradhi hayo.
