Mwenyekiti wa Chama Cha Wanajeshi Wastaafu Tanzania (MUWAWATA), – Assedy Rajabbu ameihakikishia Serikali kuwa chama hicho kina uwezo wa kuanzisha Viwanda vya mazao ya kilimo na mashamba makubwa ya mfano kikipewa nafasi.
Assedy ametoa kauli hiyo wakati Wanajeshi hao Wastaafu walipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, -Japhet Hassunga.
Wakati wa mkutano huo, Waziri Hasunga amewashauri Wanajeshi hao Wastaafu kujihusisha na uzalishaji wa mazao ya Kilimo.