Rais Magufuli aeleza alivyonyweshwa Sumu

0
845

Rais John Magufuli ameelezea namna alivyonusurika kifo baada ya kunyweshwa sumu akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake kama Waziri wa Ujenzi na kumshukuru Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa kuendelea kumuami na kumpa ulinzi.

Akihutubia jijini Dar es salaam wakati akizindua kitabu cha maisha ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin Mkapa, kilichopewa jina la Maisha yangu, Kusudio langu Rais Magufuli amesema kuwa, amejifunza mambo mengi sana lakini utendaji kazi wake ndio ulisababisha atake kuuwawa kwa kunyweshwa sumu baada ya Mzee Mkapa kutamka kuwa yeye (Rais Magufuli) ni askari wa Mwamvuli namba moja.

Rais Magufuli amesema, aliandika barua ya kujiuzulu Uwaziri kutokana na maswahibu hayo lakini Mzee Mkapa alimkatalia na kumtaka akafanye kazi.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema, amejifunza mambo mengi kutoka kwa Mzee Mkapa na anajivunia kufanya naye kazi katika Serikali.

Rais Magufuli amesema, angependa kuona na Viongozi wengine wanaandika vitabu vyenye historia zao ili na vijana wengine wajifunze kutoka kwao.