Rais John Magufuli leo anazindua kitabu cha maisha binafsi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mzee Benjamin Mkapa.
Sherehe za uzinduzi wa kitabu hicho zitafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt Jakaya Kikwete na Viongozi wengine Wakuu Wastaafu, Mawaziri, Mabalozi, Wabunge na Viongozi wa Taasisi mbalimbali.
Kitabu hicho kinachojulikana kwa jina la ‘My Life, My Purpose’, kinaelezea historia ya Rais Mstaafu Mkapa kuanzia alipozaliwa, safari yake ya masomo, safari ya kisiasa ikiwemo uongozi wa nchi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005 na pia mchango alioutoa kwa Taifa na Kimataifa katika masuala ya uongozi.
Sherehe za uzinduzi wa kitabu hicho zitatangazwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao mbalimbali ya kijamii.