Liverpool wakiwa nyumbani Anfield wametoka na ushindi wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Manchester city katika mchezo wa 12 wa ligi kuu England
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Fabinho dakika ya 6, Mo Salah dakika ya 13 na Sadio Mane dakika ya 51 huku bao lakufutia machozi kwa Manchester city likifungwa na Silva dakika ya 78
Kwa matokeo hayo Manchester city imeshuka hadi nafasi ya 4 ikibaki na alama 25 huku Liverpool ikiendelea kubaki kileleni baada ya kuongeza alama 3 na kufikisha point 34
Katika mchezo wa awali wa ligi hiyo Manchester United imeibamiza Brighton & Hove Albion mabao 3 kwa 1 nakufikisha alama 16 ikishika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi Kuu England