Nchi za NORDIC zakaribishwa kuwekeza Afrika

0
184

Rais John Magufuli ametoa wito kwa nchi za NORDIC kuwekeza katika nchi za Afrika, kwa kuwa nchi hizo zina maeneo mengi na mazuri kwa ajili ya Uwekezaji.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akifungua kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na NORDIC.

Amesema kuwa, nchi za NORDIC zina uzoefu mkubwa katika Uwekezaji katika maeneo mbalimbali, hivyo ni vema zikawekeza zaidi katika nchi za Afrika ili nazo ziweke kupiga hatua kimaendeleo.

Kwa upande wa Tanzania Rais Magufuli amesema kuwa, tayari imeweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuvutia Wawekezaji ikiwa ni pamoja na kuanzisha Wizara maalum kwa ajili ya kushughulikia Uwekezaji iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kuweka miundombinu rafiki katika maeneo ya Uwekezaji.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa, Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi za NORDIC ambazo zimepiga hatua kubwa katika ujenzi wa viwanda vya usindikaji wa mazao, ili ipate utaalamu katika ujenzi wa viwanda vya aina hiyo.

kikao hicho cha Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na NORDIC kimehudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali Wastaafu akiwemo Rais wa awamu ya Pili wa Tanzania, – Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa awamu wa Nne Dkt Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba.

Nchi za NORDIC ni Denmark, Finland, Norway, Sweden na Iceland.