Tanzania kuendelea kushirikiana na Nchi wanachama SADC

0
198

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema serikali ya TANZANIA itaendelea kushirikiana na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika -SADC kuhakikisha huduma za afya zinamfikia kila mwananchi ili kuwa na mataifa yenye wananchi wenye afya njema kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo.

Akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa afya wa SADC jijini DSM, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema ni jukumu la kila nchi wanachama wa SADC kuhakikisha  huduma za afya zinapatikana kwa urahisi
pamoja na kuanzisha bima ya afya kwa kila mwananchi.