Newcastle na West Ham zamuwinda SAMATTA

0
1258

Timu za Newcastle United na West Ham United za Ligi ya England zimeonyesha nia ya kumtaka nahodha wa timu ya Soka ya Tanzania ( Taifa Stars), – Mbwana Samatta.

Samatta mwenye umri wa miaka 26, ni mshambuliaji wa Klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji.

Tayari Samatta amepachika mabao mawili kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku moja akiwafunga mabingwa wa Ulaya Liverpool siku ya Jumanne, katika mchezo uliomalizika kwa Liverpool kushinda mabao 2-1 dhidi ya Genk

Katika Mkataba wake kwenye Klabu ya Genk, kuna kipengele cha uhamisho chenye thamani ya Pauni Milioni Kumi

Nahodha huyo wa Stars amefunga magoli sita katika mechi 13 za ligi msimu huu.