Yanga yaachana na Zahera, Mkwasa akabidhiwa timu

0
1070

Uongozi wa klabu ya Soka ya Yanga umetangaza rasmi kuachana na Kocha wake Mkuu Mkongomani Mwinyi Zahera na Benchi zima la ufundi la klabu hiyo.

Nafasi ya Zahera amekabidhiwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa “Master” kuanzia hii leo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Soka ya Yanga Dkt Mshindo Msolla ametangaza maamuzi hayo ya uongozi wa Yanga mbele ya Waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Mwinyi Zahera alikabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa Mzambia George Rwandamina na alikua na mkataba na Yanga hadi Septemba 2020.