Utambuzi wa miili ya watu waliokufa maji waendelea

0
2091

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amesema kuwa utambuzi wa miili ya watu waliokufa maji kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere inaendelea hivi sasa.

Akizungumza katika eneo ilipotokea ajali hiyo, IGP Sirro amewataka Watanzania wote kuendelea kuwa watulivu wakati shughuli hiyo ikiendelea na kusimamiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mwanza.

Kivuko cha MV Nyerere kinachotoa huduma zake kati ya Bugorora na Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza kilizama Alhamisi Septemba 20 mwaka huu kikiwa katika safari zake za kawaida.

Habari kutoka mkoani Mwanza zinasema kuwa kati ya watu 37 waliookolewa baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kulazwa hospitalini wakipatiwa matibabu, 25 wameruhusiwa.