Moto wazuka kwenye treni na kusababisha vifo

0
834

Zaidi ya watu Sabini wamefariki Dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya moto mkubwa kuzuka katika treni moja ya abiria nchini Pakistan.

Moto huo ulianzia jikoni ndani ya mgahawa wa treni hiyo, baada ya jiko la gesi kulipuka.

Habari kutoka nchini Pakistan zinaeleza kuwa, idadi ya watu waliokufa kutokana na moto huo inaweza kuongezeka, kwa kuwa zoezi la uokoaji bado linaendelea.

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa, abiria waliokuwa ndani ya treni hiyo walishikwa na taharuki baada ya treni hiyo iliyokua kwenye mwendo kasi kushika moto, hali iliyowafanya baadhi yao kuamua kuruka.

Polisi nchini Pakistan wanaendelea kufanya uchunguzi kuhusu ajali hiyo ya treni, iliyokua ikitoka katika mji wa Karachi kuelekea mjini Islamabad.