Chicago Bulls washindwa kutamba kwa Cavaliers

0
835

Wakongwe Chicago Bulls wameshindwa kutamba mbele ya Cleveland Cavaliers, na kunyukwa alama 117 kwa 111 katika mwendelezo wa michezo ya Ligi Kuu ya kulipwa ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA).

Tristan Thompson ameifungia Cavaliers alama 27 na kucheza mipira iliyorudi yaani Rebounds Kumi huku Kevin Love akiifungia alama nyingine 17 na kuzima ndoto za Bulls kuibuka na ushindi katika uwanja wa ugenini.

Matokeo mengine New York Knicks wamepoteza kwa alama 95 kwa 83 mbele ya Orlando Magic, wakati Indiana Pacers wakiinyuka Brooklyn Nets alama 118 kwa 108 , huku Boston Celtics wakipata ushindi wa alama 116 kwa 105 dhidi ya Milwaukee Bucks.

Oklahoma City Thunder wamepoteza nyumbani kwa kipigo cha alama 102 kwa 99 kutoka kwa Portland Trail Blazers, nao Minnesota Timberwolves wakishindwa kutamba mbele ya Philadelphia 76ers kwa kunyukwa alama 117 kwa 95, na Bingwa mtetezi Toronto Raptors ameendeleza ubabe kwa kuinyuka Ditroit Pistons alama 125 kwa 113.