Mamia ya Waandamanaji nchini Chile, wamerejea tena katika mitaa ya
nchi hiyo kuendelea na maandamano ya kupinga Serikali, licha ya
Serikali ya Rais Sebastian Pinyera wa nchi hiyo kufanya mabadiliko
katika Baraza la Mawaziri.
Rais Pinyera aliahidi kufanya mabadiliko katika Wizara Tisa na Serikali yake, jambo ambalo amelitekeleza katika kipindi cha siku chache zilizopita, lakini Waandamanaji hawajaridhika na mabadiliko hayo na kuendelea na maandamano.
Waandamanaji hao walikuwa wakimshinikiza Pinyera na Baraza lake lote
la Mawaziri kuachia madaraka, kwa madai kuwa Serikali yake imekithiri
kwa vitendo vya rushwa.