Kambi ya Elimu Simiyu Yafungwa

0
154

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, amefunga rasmi kambi ya Elimu kwa ajili ya Wanafunzi wa kidato cha Nne kutoka wilaya zote za mkoa wa Simiyu.

Kambi hiyo ya siku Sitini, ilishirikisha Wanafunzi 1,512 na lengo lake ni kuwaandaa Wanafunzi wa mkoa wa Simiyu wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha Nne na kuongeza kiwango cha ufaulu wa Wanafunzi wa mkoa huo.