Lugha ya KISWAHILI kuendelea Kuenea Zaidi DUNIANI

0
229

KAMPUNI ya China Federation of Internet kwa ushirikiano na Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes zimeendesha Kongamano la utamaduni na umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii (China – Tanzania Cyber Cultural Exchange) Jijini Dar es Salaam huku Kampuni hiyo ya StarTimes ikizindua Programu Tumishi (application) kwa Lugha ya Kiswahili

Akiongea Katibu Mkuu wa mtandao China Federation of Internet, Zhao Hui, amesema amevutiwa na kasi ya watanzania kutumia mitandao ya kijamii ambayo inachangia kuwaleta watu pamoja.

Pia amesema mitandao ya kijamii sasa imefungua mlango mpya wa kukuza kiswahili na kuwa chombo kingine cha habari kwa kufanya watu waweze kutuma ujumbe mfupi wa maandishi bure na kupata mrejesho wa haraka