Mwanariadha Alphonce Simbu, amefanikiwa kupeperusha vema bendera ya Tanzania katika mashindano ya Majeshi ya Dunia huko nchini China na kujinyakulia medali ya Fedha
Mwanariadha huyo kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ameshika nafasi ya Pili baada kukimbia kwa saa 2: 11.16 huku akiwashinda wakimbiaji wengine 95 kutoka nchi zaidi ya Thelathini.
Mshindi wa Kwanza ni Luche Sumi kutoja Bahrain aliyekimbia kwa muda wa saa 2:08.28 na mshindi wa Tatu ni mwanariadha kutoka Rwanda, – John Hakizimana akiyekimbia kwa karibu nyuma ya Simbu kwa saa 2:11:19.