Boeing 787 yapokelewa , Rais awapa neno ATCL

0
304

Rais Dokta JOHN MAGUFULI amewataka watendaji wa Kampuni ya Ndege ya
TANZANIA – ATCL kufanya kazi kwa weledi na kutoa huduma bora kwa wateja.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JULIUS NYERERE
Jijini DSM mara baada ya kupokea ndege ya pili aina ya Boeing
787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Kampuni ya.l Ndege ya ATCL Rais MAGUFULI amewataka watendaji wa shirika hilo kuhakikisha wanaondokana na malalamiko kutoka kwa wateja ikiwemo
huduma zisizoridhisha, lugha mbovu kwa wateja na kuahirishwa kwa safari bila mpangilio na sababu za msingi.