Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza, akikagua kazi mbalimbali za Sanaa na Utamaduni alipotembelea mabanda ya Wajasiriamali wakati wa kufunga Tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lililofanyika kwenye Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Wakati wa Tamasha hilo, sanaa mbalimbali zimekua zikioneshwa ikiwa ni pamoja na sarakasi, uchoraji, ngoma, maigizo na nyimbo za makabila.
Tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilifunguliwa Oktoba 19 mwaka huu na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe.