Idara ya Uhamiaji mkoani Morogoro, inawashikilia Wahamiaji 11 Raia wa Ethiopia, kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.
https://www.youtube.com/watch?v=IgdzymMogY0&feature=youtu.be
Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Morogoro, – Angelina Shija amesema kuwa, Wahamiaji hao wamekamatwa katika maeneo ya Mikumi na Dakawa wakiwa katika harakati za kuelekea nchini Afrika Kusini.
Shija amesema kuwa, Idara ya Uhamiaji itaendelea kuwakamata Raia wote wa kigeni ambao wamekua wakiishi nchini bila ya vibali.